Staa wa R&B wa Marekani, Trey songz ametua jijini Nairobi, Kenya tayari kwa ajili ya msimu wa nne wa Coke Studio.
Kilichowavutia watu zaidi ni pale staa huyo alipoamua kutumia usafiri wa daladala za nchini humo maarufu kama ‘Matatu’
Hii ni mara ya kwanza kwa mshindi huyo wa Tuzo za Grammy kutua Afrika Mashariki, Trey atashirikiana na mastaa wa Afrika ikiwemo Nyashinski (Kenya). Yemi Alade (Nigeria), Vanessa Mdee (Tanzania), Rema (Uganda), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), na Emtee (South Africa).
Story By: @Joplus_
Source: Perfect255.com