“SALOME” YA DIAMOND YAVUNJA REKODI YA KUWA NA VIEWERS WENGI ZAIDI YA MIL.1 KWA SIKU 2.

Miezi 2 iliyopita msanii mkali kutoka Tanzania Diamond Platnumz alivunja rekodi barani Afrika kwa wimbo wake wa “Kidogo” ambao aliwashirikisha P-Square kupata viewers zaidi ya Million 1 katika mtandao wa Youtube ndani ya siku 4 tu.

Ila leo mkali huyohuyo anarudi tena kuivinja rekodi ambayo aliiweka yeye mwenyewe miezi miwili iliyopita. Ni video ya wimbo wa Salome ambayo imefikisha viewers zaidi ya million 1 kwa muda wa siku 2 tu.

Instagram photo by Chibu Dangote_BKnMni_jNEy - JPG

Inaonyesha dhahiri ni kiasi gani wimbo wa Salome umepata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, na wakubwa wa mambo wameutabiri wimbo huo kuishi muda mrefu sana na kufika mbali zaidi kutokana na mahadhi yake.

Story By:@Joplus_

Source:Perfect255.com