MTOKO WA BEYONCE VMA 2016 HAUJAWAHI KUTOKEA

597193262
Beyonce ni Moja ya wasanii ambao walikuwa wanapita kwenye Red Carpet ya MTV VMA 2016 na kukamata macho ya watu wengi na kufanya midomo ya watu kuwa wazi kwa muda, 100% hili gauni alilovalia ambalo linamuonekano kama wa Malaika hivi, huku kwenye mabega kukiwa kumezungukwa na kama Manyoya flani hivi ambayo yanavutia, hili gauni limetisha kinoma noma.

Ukiachana na Bey kwenye mitupio hiyo, Blue Ivy naye alikuwa sambamba na Mama yake akiwa anafuata fashion za Bimdash wake.

Hiyo ilikuwa ni kwa upande wa Red Carpet, Sasa Beyonce aliamua kuonyesha ni jinsi gani alivyokuwa hana ziki kwenye upande wa Fashion, Kila Tuzo ambayo alikuwa akipokea alikuwa anakuja na Fashion nyingine ambayo bado ikawa inazidi kuteka bongo za watu waliohudhuria tamasha hilo.
Hili ni Gauni ambalo linataka kufanana Kama na yale ambayo tunayatumia kwenye harusi zetu, lakini sio bhana Hiyo ni Fashion tu, Hapa alikuwa anapokea tuzo yake ya VIDEO OF THE YEAR “FORMATION”

Unajua Beyonce alikuwa akiwapa raha tu watazamaji na mashabiki wake kila anapokuwa anakuja kwenye steji na fashion nyingine ambayo lazima mate yakutoke kidogo kwa mavazi jinsi yanavyomkaa mwanamama huyo.
Hebu niambie hapo kwa upande wa wasanii wetu nani huwa anafunika kama Beyonce.@Joplus_

Source: www.rahatupu.us