Issue iliyogonga vichwa vya habari kwenye site nyingi wiki hii ni ngoma mpya ya Diamond Platnumz, inayoitwa Salome, ambayo kwa mara ya kwanza iliimbwa na mkongwe wa muziki wa asili nchini, Saida Karoli mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Mtindo wa msanii kurudia wimbo wa msanii wa kitambo upo ulimwenguni kote na hapa Bongo tunakutana na wasanii kama Mwana FA
aliyewahi kurudia wimbo wa Bi. Kidude, Ali Kiba aliyewahi kurudia wimbo wa Issa Matona, Ben Pol naye aliwahi kurudia wimbo wa Less Wanyika na Lady Jaydee aliyeimba Siwema.
Hali imekuwa tofauti kwa Diamond Platnumz
kwani wimbo huo wa Salome umeweza kuwavutia watu wengi zaidi pengine kuliko zilizotangulia kufanywa na wasanii wengine kabla yake.
Ukiacha yote hayo, ushiriki wa mrembo Hamisa Mobeto kama mmoja wa ma-Video Queens katika kichupa hicho, umeamsha mjadala wa muda mrefu kuhusu kuwepo kwa fununu za wawili hao kutoka kimapenzi.
KWANINI TETESI?
Tukio la kwanza lililosababisha wapenda burudani waanze kuhisi kuna kitu kinaendelea kati ya Hamisa na Diamond ni siku ya sherehe ya kuzaliwa ya mama yake na Diamond, Bi. Sandra ambayo ilifanyika Julai, mwaka huu nyumbani kwa staa huyo, Madale, Dar na kuhudhuriwa na Hamisa.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo mastaa kadhaa wa Bongo, Hamisa alizua maswali baada ya kuonekana kuwa karibu mno na mama mzazi wa staa huyo na dada yake anayeitwa Asma.
Licha ya mpenzi wa Diamond, Zari kuwepo
kwenye sherehe hiyo, hakuwa habari kubwa sana kama ilivyokuwa upande wa Hamisa, kutokana kuonekana kujishughulisha kwenye shughuli za kifamilia zilizokuwa zinafanywa na mama na dada wa Diamond.
Kiashiria kingine kilichowaaminisha wengi kuwa Hamisa anataka kumpindua Zari ni picha zilizosambaa mitandaoni zikiwaonyesha wapo kwenye chumba kimoja huko Afrika Kusini.
Tangu video imetoka leo ina siku sita lakini mpenzi wa Diamond, Zari hajaposti chochote kuonyesha kumsapoti mpenzi wake, huku ikidaiwa kuwa uwepo wa Hamisa kwenye video hiyo umechangia mrembo huyo wa Kiganda kutoposti chochote.
VIDEO YA SALOME
Baada ya viulizo hivyo kutanda kila kona,
Swaggaz lilimsaka Hamisa na kufanikiwa
kuzungumza naye, ambapo hapa alifunguka
kuhusu tetesi za uhusiano wake na Diamond na mengine yanayozungumzwa mitaani.
“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu ambao watu
wamekuwa wakiongea wanayoyajua kuhusu mimi na Diamond. Nadhani video hii imetoa jibu ya kwa nini nilikuwa karibu na Diamond.
“Ile ni kazi na nimelipwa, siwezi kuogopa kuwa karibu na mtu fulani kikazi eti kisa nitaambiwa natoka naye,” anasema Hamisa.
UKARIBU NA FAMILIA YA DIAMOND
“Nashangaa watu wanavyounganisha matukio,
ile video ya Salome tuliifanya mwezi Aprili kwahiyo ukaribu wetu wa kikazi na Diamond ulikuwa tangu kipindi hicho, sasa business partner (mshirika wa kibiashara) wako akiwa na jambo huwezi mpa sapoti? Labla walitaka nisiende na mimi sikuwa na sababu ya kutokwenda kwenye birthday ya mama yake. Kuhusu Asma yule ni rafiki yangu,” alisema Hamisa.
KUKAA CHUMBA KIMOJA VIPI?
“Nimeanza kufahamiana na Diamond zamani,
siku ya kwanza ni siku alipokuwa anazindua video ya My Number One pale Serena Hotel, toka hapo tumekuwa marafiki na tunaheshimiana tofauti na watu wanavyodhani.
“Kama nilivyosema hapo awali siwezi kuogopa maneno ya watu wakati najua hayaniongezei chochote. Ile ilikuwa ni Afrika Kusini kuna sehemu inaitwa Capital, huwa wanafikia Wabongo wengi, vyumba vyote vinafanana kwa hiyo mimi nilikuwa kwenye chumba changu na
Diamond na familia yake walikuwa kwenye
chumba chao, sasa kulala wote hapo kunatoka wapi?” anahoji hamisa.
MAAJABU YA SALOME
Inawezekana Diamond akawa amevunja rekodi
Afrika, kwa sababu siku ya nne tu tangu
alipoachia video ya wimbo huo katika mtandao wa YouTube, tayari imeshatazamwa na watu milioni moja, jambo ambalo ni adimu kutokea kwenye ulimwengu huu wa ushindani.
Hiyo inawezaa kuwa ni safari ya kuelekea
kushinda tuzo kibao za kimataifa kama kawaida
yake.
Story by:@Joplus_
Source:Perfect255.com