WEMA SEPETU AKANA KUMJUA MANFONGO.


Leo ni siku ya 3 ya muendelezo wa sakata zito ambalo lime make headlines kinoma katika mitandao ya kijamii.
Ni sakata linalo muhusisha mama mzazi wa mwanadada Wema Sepetu na msanii mchanga ambaye amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa kufanya muziki wa kisingeli (Man Fongo).
Jana tuliweza kuyasikia mapovu ya Mama Wema na mgomvi mwenzie Man Fongo ila leo Gossip Master Soudy Brown ameamua kumvutia waya ambaye anaseekana ndio chanzo cha sakata hilo.
Lakini hapo jana mwanadada Wema alipoona kama mama yake anakuwa ni gumzo sana katika mitandao ya kijamii akaona isiwe kesi ngoja amvutie waya Soudy Brown na kumwambia kuwa aachane na hizo mambo za kumchoresha mama yake.Ni mapovu sio ya kitoto yamemtoka Bi Dada Wema Sepetu na amekana kabisa yeye kumjua Man Fongo wakati siku chache zilizopita alipost katika account yake ya Snapchat akiwa anaserebuka na ngoma ya “Hainaga Ushemeji”.
Isiwe kesi ngoja nikupe nafasi ya kuitazama na kusikiliza hii video yenye ubuyu wote unaokiki town kwa sasa.


Story By: @Joplus_

Source: Raha za walimwengu