SAM MSAGO AJISOGEZA KARIBU NA RUNGU HILI KALI KUTOKA BASATA

Mtangazaji wa East Africa Radio na TV napia ni msanii,Huenda sammisago akaingia kwenye list ya watu waliokumbana na Rungu la Baraza la sanaa Tanzania basata siku chache zijazo.
“Vyura na madanga”Hii ni ngoma ya 3 ya sammisago baada ya #Nimepania ft benpol na Balling n chilling ft marehemu #udeude, lakini jina lake tu tayari ni utata wakati mashabiki wakisubiria video yake. “Vyura na madanga”jina hili linarudisha akili za watu nyuma kwenye wimbo wa #Snura#chura ambao ulifungiwa muda mfupi tu baada ya video yake kuachiwa miezi kadhaa iliyopita.Snura mwenyewe alipousikia wimbo huu alimwambia ajipange kukumbana na #Basata.

Kupitia #Planetbongo sammisago amesema hawezi kuogopa kuachia video ya wimbo huo kwa kuogopa kufungiwa na baraza la sanaa la Taifa (Basata) ,kwa kuwa anachoangalia ni kutengeneza video itakayofanana na wimbo husika.
“Kama director akisema hapa akae bebe mmoja mkali acheze nguo yake ikiwa imeloana basi itakuwa hivyo…”alisema sam na kuongeza kuwa Basata inabidi wajue sanaa huwa haiwekewi mipaka na Basata.

Kwa mujibu wake yupo katika mipango ya kushoot video hiyo akisisitiza atafanya kile sanaa yake inachotaka.
Sammisago ni mtangazaji wa Eatv lakini alikuwa msanii kabla ya kuwa mtangazaji na amesema ni kitu anachopenda kukifanya.@Joplus_

Source: www.rahatupu.us