MATUMAINI MAPYA YA TIBA YA SARATANI

Uchunguzi wa geni wa Tasmanian devils umebaini uwezo wa haraka wa kutibu maambukizi ya saratani ya uso inayotishia wanyama hao.

Ikiwa ni moja kati ya aina tatu za maambukizi ya saratani yanayoweza kuambukiza , uvimbe huu umewauwa asilimia 80% ya wanyama hao wa mwituni katika kipindi cha miaka 20 .

Watafiti waliangalia sampuli kutoka kwa wanyama 294, wanaoishi katika maeneo tofauti, kabla na baada ya ugonjwa huo kufika.

Makundi mawili madogo ya devil yalionekana kuwa na mabadiliko ya haraka na kuwa na geni zenye uwezekano mkubwa wa kupambana na geni za saratani.

NI aina mbili nyingine zaidi za saratani zinazotambuliwa na wanasayansi.

Uvimbe kama huo ulisambazwa kwenye viungo vya uzazi vya mbwa walipokutana na wanyama hawa miaka 11,000 ; na mwingine uligundulika mwaka 2015 miongoni mwa wanyama hao maeneo ya fukwe za kusini magharibi mwa Marekani

Ugonjwa wa uvimbe wa uso wa Devil (ulionekana kuwatokomeza kabisa kwenye ramani ya dunia

Akizungumza na waandishi wa habari , mmoja wa waandalizi wa uchunguzi huu DK Paul Hohenlohe alisema kuwa yeye na wenzake walikuwa katika mazingira ya kipekee ya kuwachunguza Tasmanian devil walioweza kupambana na saratani – kwasababu sampuli zao zilitengwa kwenye sehemu tofauti na ziliangaliwa kuanzia mwaka 1999 hadi 2014.

Kwa kutumia njia ya kuchunguza msururu wa vinasabavilivyochukuliwa hivi karibuni waliweza kuangalia mabadiliko kwenye geni zote.@Joplus_

Source: Muungwana Blog