DJ KHALID ATUPIA KIONJO CHA VIDEO YA WIMBO WAKE WA ‘DO YOU MIND’.

Mtu wangu wa nguvu leo nimeipata hii kutoka kwa DJ Khaled a.k.a Snapchat King ambaye ametuletea kipande cha Video yake mpya itakayotoka muda mchache ujao. Wimbo unaitwa Do You Mind ambao amewapa collabo mastar kama Nicki Minaj, Chris Brown, August Alsina, Rick Ross, Jeremih na Future.

Mwezi uliopita DJ Khaled aliweka picha za behind-the-scenes kuptia Snapchat akiwa location kushoot video ya wimbo huo. Kwa mujibu wa DJ Khaled ataiachia kwenye sherehe za BET Hip-Hop Awards.

Story by:@Joplus_

Source: Millard Ayo.