MSAGA SUMU AKIRI UPINZANI NI MKALI KWENYE SINGELI

Najua nikiongelea muziki wa Singeli na wakali wa muziki huo kwa zamani utamwongelea mfalme wa muziki huo Msaga Sumu lakini kwa sasa kumekuwa na ushindani mkubwa kutokana na wasanii waliongezeka kwenye fani hii nikiongelea Manfongo na Sholo Mwamba pamoja na wengineo.

Camera za Ayo TV na Millardayo.com zimeweza kumpata Msaga Sumu na ameongea haya juu ya ushindao huo>>‘Naweza nikasema wasanii wengi wanakuja na me binafsi napenda navyoona visingeli inakuja juu napenda sana kwasababu napata changamoto flani na kiukweli wanakuja vizuri hata me mwenyewe nafarijika lakini ….’ Reporter:@Joplus_

Source: Millard Ayo