HARMONIZE: SIWEZI KUOGOPA COLABO

Harmonize

Msanii wa kundi la WCB Harmonize amesema kwa sasa hayuko tayari kufanya colabo na kuwapa watu muda wa kuwatengenezea ushindani kati yao.

Akipiga story ndani ya eNews amesema “Colabo ni kubadilishana mashabiki kwa wakati nafanya colabo na Diamond nilikuwa nikilenga kuwa kuna mahali muziki wa Diamond umefika wa kwangu haujafika na pia Diamond ana’hit’ nyingi kwa hiyo likuwa ni mpango wa kufikisha muziki wangu mbali”
“Ningekuwa naogopa colabo basi ningeogopa kufanya colabo na Diamond kwa kuwa ni muimbaji mzuri kuliko Diamond lakini niliamua kukaza tu ili kufika mbali, lakini pia inabidi tupate muda tutengeneze wimbo mzuri ili kitoke kitu kizuri”.aliendelea kusema Harmonize.

Pia hakusita kuelezea maswala ya mahusiano yao na Wolper akisema “siku zinavyozidi kwenda binadamu anapata mawazo mapya pamoja na kukua lakini pia nafikiri ilikuwa ni upya ndo maana kila siku tulikuwa tukifanya mambo mbalimbali kwa kuwa wote tulikuwa tukitamaniana”.

Reporter:@Joplus_

Raymond ‘Rayvan’
Source: Muungwana Blog