GURUDUMU LA KIJIJI CHA MAISHA PLUS LAANZA RASMI

Masoud na Babu wa Kijijini wakiteta jambo

 Vijana 30 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki, Jumapili hii waliingia rasmi kwenye kijiji cha shindano la Maisha Plus.

Kuwasili kwa vijana hao katika kijiji hicho ambacho hakijulikani kilipo, kulikuwa kukirushwa live kupitia kituo cha runinga cha Azam Two. Wakiwa na mabegi yao mkononi, washiriki hao walipokelewa na mwanzilishi wa kipindi hicho, Masoud Kipanya huku wakiwa wamefunikiwa vitambaa vyeusi machoni.

Babu akikagua himaya yake

Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30. Washiriki wote watapewa shilingi 7,000 kwa wiki ili kujikimu wakiwa kwenye kijiji hicho kilichopo katikati ya msitu. Lengo la kupewa shilingi 1,000 kila siku ni kuwafunza maisha ya waafrika wengi ambao huishi chini ya dola moja kwa siku.

Hakuna nyumba kwenye kijiji hicho na hivyo watatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe za kuishi.

Reporter: @Joplus_

Tazama picha zaidi hapo chini.

 Washiriki wakiwa wamefunikwa vitambaa vyeusi usoni mwao

 Babu akimwelekeza jambo mmoja wa washiriki

 Babu akiwa kazini
 Masound Kipanya akitoa maelekezo kwa washiriki

 Washiriki 30 watalazimika kuishi maisha magumu kuwania kushinda shilingi milioni 30

 Washiriki hawatajua mahali walipo muda wote watakaokuwa kijijini hapo

 Washiriki watajipikia wenyewe kwa bajeti ya shilingi 1000 tu kwa siku

Source: Muungwana Blog