MWANA FA ASEMA ANATAMANI AFANYE COLLABO NA CHRISTIAN BELLA PAMOJA NA TORY LANES WA MAREKANI.

Rapa mkongwe kwenye muziki wa hip hop Tanzania Mwana FA amefunguka na kusema kuwa anatamani sasa kufanya collabo na msanii Christian Bella Obama kwa wasanii wa ndani huku akitamani kufanya kazi na msanii Tory Lanes kutoka Marekani.

Mwana FA amesema hayo kupitia ‘Account’ yake ya Twitter baada ya kuwapa nafasi mashabiki zake kumuuliza maswali na yeye kuyajibu, mbali na hilo Mwana FA amedai kuwa toka ameanza kufanya muziki na kutoa ngoma kibao kali lakini yeye ngoma zake tatu kali anazozikubali zaidi ni pamoja na ‘Mabinti, Alikufa kwa ngoma, pamoja na Mfalme’.

Wakati ambapo mashabiki wengi walikuwa wanategemea kusikia ‘Remix’ ya ‘Asanteni kwa kuja’, Mwana FA amethibitisha kuwa remix hiyo inakuja muda si mrefu kutoka sasa na kusema kila kitu kimekamilika ila anasubiriwa msanii mmoja aingize ‘verse’ yake kwani huyo msanii yupo busy kidogo na mambo yake mengine.

“Kuna ‘mzee mmoja’ tunangoja verse yake,
akimaliza huyo itakuwa tayari..sema ana
majukumu mengi kidogo” alisema Mwana FA.

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com.