PENZI LA DRAKE NA RIHANA LAZIDI KUNOGA.

imagesRihanna na Drake wameamua kuanika uhusiano wao ambao umekuwa siri kwa muda wa miezi kadhaa.

Baadhi ya wanahabari na mashabiki za mastaa hao wameeleza kuwa, tattoo hiyo inaashiria jambo flani kati yao ambalo bado hakijajulikana.

Wawili hao wamekuwa gumzo kwa sasa kwenye vyombo vy habari na mitandao ya kijamiitangu walivyoanika uhusiano wao kwenye tuzo za usiku wa Jumapili ya tuzo za VMA.

Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa Drake na  Rihanna walitumia usiku huo kupeana mahaba mazito ikiwa ni pamoja na kuimba na kucheza pamojakwenye meza yao ya VIP. Lakini wakati Drake akiimba jukwaani, Rihanna alikuwa akimtazama na kucheza kimoyo moyo.Licha ya kujiachia kimahaba, Rihanna na Drake waliondoka kila mtu kivyake. Rihanna aliwahi kuondoka mida ya saa 8:00 usiku wakati Drake alifuata nusu saa baadaye.Baadaye tena wakaonekana na kuondoka tena saa 9:30 usiku kwa kuachana dakika tano pekee.

Story by:@Joplus_

Source: Global Publishers.