DRAKE ANUNUA NYUMBA YA JIRANI ZAKE KWA DOLA MIL.3.

Msanii Drake ameamua kumdondoshea ofa ya dola million 3 jirani yake ambaye alikuwa akipeleka malalamiko katika kituo cha polisi mara kwa mara kwa madai ya kukerwa na kelele za msanii huyo.

Inasemekana msanii Drake alikuwa akifanya Party za usiku katika nyumba yake hiyo na kusababisha kelele kwa majirani zake kitu ambacho kilikuwa kina wakera majirani hao na kuwafanya kwenda kumshtaki mara kwa mara kwa kelele zake hizo kitu ambacho Drake aliona sio kesi akiwatembezea mtonyo na kuweza kutemana na eneo hilo ili aweze kujiachia na mambo yake kwa nafasi.

Inasemekana nyumba hiyo baada ya Drake kuinunua kwasasa anaitumia kama nyumba ya kufikia wageni. Itazame hapa.

drake_new_manshion

drake_new_manshion1

drake_new_manshion2

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com