Kwa muda mrefu, meneja wa Diamond, Babutale amekuwa shabaha ya wasanii wengi wanaomtuhumu kuwa chanzo cha anguko la baadhi ya wasanii nchini.
Rappers wengi wamesikika wakimchana meneja huyo kwenye mashairi yao. Lakini sasa rapper Nikki Mbishi, ameenda mbele zaidi kwa kuandika wimbo ambao asilimia 100 unamchana Babutale. Kupitia mitandao ya kijamii, rapper huyo amesambaza mashairi ya ngoma hiyo ambayo bado haijatoka.
Haya ni mashairi yake:
Verse 1:
Naitwa kaka meneja mzee wa fitina tangu kale/
Mr. Middleman Boss tough wallet Babu Talent/
Natoka Manzese Tip Top Connection/
Huku hatupendi ngumu labda hip hop commercial/
Madee alikuwa anarap nikamwambia hiyo haiuzi/
Siku hizi anaimba video anashootia Sauzi/
Anabang sana clouds ngoma kali zinapigwa/
Huku Daudi wa kota akiongoza wakali wa media/
Nimekuwa mdananda kwenye game before/
Enzi hizo brother ndo anamtoa MB Dogg/
Z Anto Gorilla killers same thing bro/
Japo wengi wamefall from the fame to being broke/
Msinilaumu mlipata pesa mkacheza/
Kama Tunda Man sijui hata wapi alipowekeza/
Nina pesa magari mijengo biashara kubwa/
Siwezi bishana na Baghdad wala Afande mla msuba/
Verse 2:
Napiga tu mabao kila mpira wavuni/
Nina connection kibao kwenye kila kampuni/
Ukiniletea hasira za Q Chillah na uhuni/
Nakuacha bila bila kapuni mila kanuni/
Nipo pia kwenye academy za kuandaa tuzo/
Hip Hop nilimpa Nay ili hali hazijui nguzo/
Aliondoka kwa pozi akarudi kwa chozi Dogo Janja/
Singeli inabamba siku hizi uswazi tozi Sholo Mwamba/
Na Man Fongo nataka niwachukue/
Niwafanyie promo majina yao yakue/
Watokezee EaTv Cheche za Duwe/
Ndoto nifufue milango ya fursa nifungue/
Kifupi nimeshika kila media/
Muziki ni biashara huwezi bisha bila tija/
Nilimpenda Nikki Mbishi kwenye Play Boy tu/
So nifanye tena Play boy iwe play boy 2/
Verse 3:
Niko na mwanangu Gaidi Sela/
All the way from Temeke tunafaidi hela/
Tunataka Ya Moto Band wageuke barafu/
Chege na Temba TMK imbombo ni ngafu/
Mitaa haiwataki japo wapo kwa safu/
Kichaa hawanifuati nipo dampo pachafu/
Bando nasurf tu followers wakutosha/
Nikiwa na Dangote shobo nazi za kuchota/
Si unajua tena chama la wasafi/
Hip Hop sio jifanyeni wanaharakati/
Harmonize kaja jana na leo anakaa Masaki/
Anavaa mashati siku hizi hafanani kukaa Masasi/
Siko Talented ila ndo Babu Talent/
Dotto alinibatiza tena mbele ya Daz Nalej/
Na Mo Teknix Pesa ya Madafu/
Mida inakwenda bro we hesabu masaa tu/
Story by. @Joplus_
Source:Muungwana Blog