KALA JEREMIAH ATOA FURSA KWA WASANII CHIPUKIZI


Katika kuhakikisha anakuza vipaji kwa vijana msanii Kala Jeremiah ameamua kutoa fursa kupitia ngoma yake ya “Wana Ndoto”.
Kupitia ngoma hiyo ametoa nafasi kwa vijana wenye vipaji ambao wako mtaani hawajatoka kimuziki na wana ndoto za kuja kuwa wasanii wakubwa baadae watunge mistari yao kuhusu watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu lakini main point iwe wanandoto, kisha wajirekodi na wazitupie clips hizo katika kurasa zao za Instagram na waweke hashtag ya neno ya Wanandoto (#Wanandoto) kisha yeye ataziona na atai-repost katika ukurasa wake wa Insyahram.
Na kisha watu 6 ambao videos zao zitapata viewers na likes nyingi zaidi ndio watakuwa washindi na watapata nafasi na kushiriki katika remix ya ngoma hiyo ya “Wana Ndoto”
Kala Jeremiah ameiambia Perfect255 kwamba sio mara ya kwanza kwa yeye kufanya jambo hilo. Unataka kujua ni kwenye ngoma gani ambayo alifanya kitu kama hicho hapo awali? au ni kwa engo gani? Tazama hii video hapa chini ndo amefunguka kila kitu kuhusiana na jambo hilo.@Joplus_

Source: Raha za walimwengu