AY: “HIVI WATANZANIA WA MTANDAO WANAJUA KAMA UPENDO ULIKUWEPO KABLA MAISHA YA INSTAGRAM?”.

Jamii kubwa ya watu waliopo mijini kwa siku hizi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuweka maisha yao na kufanya shughuli zao mbali mbali ikiwemo biashara baada ya kuonekana ni njia rahisi ya kujitangaza.

Wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii sahihi huku wengine wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii pasipo kuwaza ni nini kitakuja kutokea baada ya kufanya unacho kifanya.

Mfano wapenzi wengi wamekuwa waki share hisia zao kwenye mitandao ya kijamii pasipokujua kuwa inawezekana kesho wasiwe
pamoja na ikabaki maumivu.

Hili tumeliona kwa baadhi ya watu maarufu ikiwa Wema Sepetu na Idris Sultan, Wema Sepetu kwa Diamond Platnumz na wengine.

aytanzania-20161004-0001

Mwanamuziki mkali wa Hip Hop komesho, AY
ametupia post kwenye account yake ya twitter nakuwauliza watu kuhusu kama ni kweli Watanzania wengi wa kwenye mitandao ya kijamii wanafahamu upendo wakweli ulikuwepo kabla ya Instagram.

Ujumbe huo ulisomeka hivi..

PicsArt_10-04-04.14.46

Hivi watanzania wa “Mitandao” wanajua kama Upendo ulikuwepo kabla “Maisha ya Instagram”?

Niwekee maoni yako hapo chini wewe unatumia IG kufanya nini, Je unashare maisha yako au la?

Story by:@Jopus_

Source: Perfect255.com