Rapper kutoka Salasala, Godzilla ambaye pia ni moja kati ya wasanii wa bongo fleva wanaounda list ya wachezaji wa soccer wa bongo fleva.
Wengine ni pamoja na captain Tunda Man, Kr Mullah, Abdu Kiba, Rich One, Stamina, Amini, H baba, Husen Machozi na wengine wengi.
Ushawai kufikiria kama Godzilla asingekuwa mwanamziki angekuwa anafanya shughuli ipi katika michezo?
Kupitia perfect255 Godzilla ameweza kufunguka na kuweka wazi anaposikia kitu mpira au michezo kwa ujumla yeye huchukulia vipi…
“Mpira nimchezo flani hivi unakufanya uwe active mda mrefu, minapenda michezo yote, napenda basket pia napenda Mpira. Lakini sana sana napenda mpira kwa sababu nimchezo flani hivi baada ya kucheza, wakati wa kulala unakuwa umerelax sana.”
Aliendelea “So nadhani mpira ningekuwa nacheza sana, kama sio Mpira, basket kwa sababu nacheza michezo yote miwili.”
“Wakati nakuwa nilikuwa napenda kujifunza kila kitu toka nipo shule, kwa hiyo timu ya mpira nilikuwepo, ya basket nilikuwepo.”
“Kila level ya Elimu nilikuwa katika timu zote mbili. Ilikuwa hainiathiri kwa sababu si unajua timu za shule yani hadi itokee shughuli maalum, kwa sababu ni ya wanafunzi wote so lazima itawahusu, kwa hiyo nilikuwa nashiriki kote.”
“Baada ya shule mziki nadhani ulichukua muda mwingi zaidi kwa sababu ni passion, ni kitu ambacho kilikuwa ndani kwa hiyo nikawa nafanya michezo kama part hivi,
Aliendelea “Uwezi kufanya vitu vyote kama passion. Eti muda wote uweke nguvu zote kwenye kila kitu. Hamna binadamu wa aina hiyo.”
“Nadhani mziki ulinichukua zaidi lakini bado Mpira na Basket nacheza.” Alimalizia Godzilla
Wiki iliyopita kulikuwa na mchezo kati ya Bongo Movie dhidi ya Bongo Fleva ambao godzilla pia alikuwa ndani ya kikosi cha bongofleva.
mchezo huo ulikuwa ni mchezo wa hisani kuchangia walio athirika na tetemeko la ardhi huko Bukoba.
Story by:@Joplus_
Source: Perfect255.com