WIZKID NA DAVIDO KUONYESHANA UBABE MITANDAONI.

Kumekuwa na uvumi unaowaohusisha mastaa Wizkid na Davido wanaofanya vizuri kwenye game ya muziki nchini Nigeria kuwa na beef ya kipindi kirefu lakini wenyewe hawakuwahi kuthibitisha hilo. Stori zinazoenea kwa kasi ni kumhusu mnyamwezi Wizkid kusaini  dili na Sony Music Global, Label ambayo mtu mzima Davido yupo.

Lakini vyanzo  vya karibu vya mastaa hao vimekanusha taarifa hizo na kusema Wizkid amesaini na Label nyingine na sio Sony Global kama inavyosemekana.

Story kubwa  ni ishu ya Davido kuacha comment kwenye post ya Wizikid ambayo mwanzo Wizkid aliuliza “D sony music deal or the EP?

Likiwa kama swali la kizushi kwa mashabiki wake ambao alitaka watabiri atakua amesaini na  na kuachia EP (Extended Play) chinii ya Label hiyo ambayo mnyamwezi Davido yupo.

Baadae Davido alikomenti kwenye picha hiyo kwa kuandika neno “BABA NLA!! (Jina la wimbo wa Wiz)

Davido Kwa Wizkid

Wizkid aliamua kubadili Caption ya Picha hiyo na kuandika neno “DON”

Angalia utofauti wa post hizi mbili za Wizkid. Hiyo ya juu ni kabla na hii ya hii chini ni baada ya mshikaji kuedit caption yake.

Kama Wizkid atakua amesaini na Sony anakua mwanamuziki wa tatau kutoka Afrika kusainiwa chini ya Label hiyo akitanguliwa na Alikiba(Tanzania) na Davido (Nigeria).

Story by:@Joplus_

Source:Perfect255.com