WEMA SEPETU KUMFUNGULIA DIAMOND KESI YA MADAI.

Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu anaandaa utaratibu wa kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kufuatia kitendo cha msanii wa Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Raymond ‘Rayvanny’ kumtumia kwenye video ya wimbo wake wa Natafuta Kiki bila makubaliano.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wema alisema amefikia uamuzi huo kutokana na Diamond kukiuka makubaliano waliyofanya awali kuhusu yeye kuonekana kwenye video hiyo. Alisema: “Diamond alinifuata na kunitaka nionekane kwenye video ya msanii wake Raymond, nikamwambia anipe milioni 10, yeye akaonesha alikuwa anataka free huku akisema mbona nilimsaidia Ommy Dimpoz.
 
 “Nilimwambia kuwa nilimsaidia Dimpoz kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada lakini yeye nilitaka anipe kiasi hicho cha pesa. “Baadaye niliongea na Martin Kadinda kuhusu kile alichotaka Diamond na pesa ambayo nilimtajia, Martin akaniambia kwa ishu hiyo hata milioni 10 ni ndogo, nikashituka na ndiyo maana hata Diamond aliponipigia tena kuhusu ishu hiyo nilimchomolea.” Wema akaendelea kudai kuwa, licha ya kwamba yeye alishakataa kuonekana kwenye video hiyo, siku ya ‘bethidei’ ya Rommy Jones alifanyiwa kitendo ambacho si cha haki.
 “Nikiwa pale kwenye ‘bethidei’ ya Rommy, bila kujua wana lao jambo, Raymond akawa anajiweka sana kwangu huku video na picha mbalimbali zikichukuliwa, sikujua kwamba kuna kitu nyuma yake, ile video ilipotoka nikashangaa nimetumika bila ridhaa yangu.
 “Ndiyo maana nimewasiliana na wanasheria wangu ili nimshitaki Diamond kwani yeye ndiye niliyezungumza naye na tukashindwana,” alisema Wema. Kufuatia tuhuma hizo, Risasi lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Raymond  ili kuzungumzia madai hayo lakini hawakuweza kupatikana mara moja. Alipotafutwa meneja wa Diamond, Salam Sharraf alisema: “Mimi sidhani kama kuna ishu hapo maana hata baada ya ile ‘bethidei’ ya Rommy, Wema aliiposti ile video kwenye ukurasa wake wa Insta kuonesha kuwa hakuwa na shida na sisi tukajua hata kwenye kuonekana kwenye ile video si tatizo.”
Story By:Joplus_
Source:Muungwana blog