JE, WAJUA AINA ZA SUMU YA NYOKA NA MATIBABU YAKE?

Asilimia kubwa ya nyoka ambao wapo kwenye mazingira yetu hua hawana sumu yaani kimsingi ukiona mtu ameng’atwa na nyoka leo afu kesho ndio akaenda hospitali baada ya mguu kuvimba basi ujue nyoka yule haukua na sumu. nyoka wenye sumu kama cobra na black mamba huua ndani ya dakika 20 baada ya kumng’ata mtu.hivyo ukingatwa na uko umbali wa mwendo  dakika 20 kutoka hospitali ujue utakufa tu.

aina za sumu ya nyoka..
cytotoxin poison; hii hushambulia seli za juu za mwili na kuziharibu au kuleta kidonda.

haemotoxin; hii husababisha damu iwe nyepesi sana na kuanza kuvuja ndani kwa ndani au damu kushindwa kuganda kama inamwagika kutoka kwenye kidonda, sumu husababisha sehemu muhimu za mwili kukosa damu na kufa kwa muhusika.

neurotoxins; hii aina ya sumu ambayo hushambulia mishipa ya fahamu, mgonjwa akiingiliwa na sumu hii hawezi kufanya chochote, hata kutikisa kidole hawezi na hufariki baada ya muda mfupi.

cardiotoxins; sumu hii hushambulia moyo wa binadamu na kuulazimisha kusimama hivyo kuleta kifo cha ghafla.

myotoxins; sumu hii hushambulia misuli yote ya binadamu na kuiharibu.

dalili baada ya kuumwa na nyoka...

  • maumivu makali sehemu iliyoshambuliwa.
  • ganzi.
  • kuvimba sehemu husika.
  • kidonda.
  • kuvuja kwa damu[isipozuiliwa huweza kuua.

mishipa ya fahamu; nyoka huyu huweza kutoa sumu kali kwenye mishipa ya fahamu ambayo husimamisha shughuli ya upumuaji na kuua kabla ya matibabu. kabla ya kufa mgonjwa huanza na dalili za kushindwa kuona, kushindwa kupumua vizuri, ganzi na kushindwa kusema.

misuli; nyoka kama rusells vipers, nyoka wa baharini na cobra huweza kuharibu misuli kabisa na kuifanya isambae kwenye mishipa ya damu hivyo kusababisha kufa kwa figo mara moja.

damu; aina ya nyoka kwa jina la boomsling huzuia damu kuganda na kuifanya iwe laini sana, mgonjwa huvuja damu ndani kwa ndani au nje mpaka kifo.

macho; nyoka aina ya cobra hurusha sumu yake moja kwa moja kwenye macho ya binadmu na kuyaharibu au kuleta upofu kiabisa.

huduma ya kwanza..

  • hakikisha mgonjwa anapumua hata kama ni kidogo
  • angalia kama kuna damu inavuja sehemu
  • hakikisha anapaata hewa ya kutosha, asizungukwe na watu.
  • mgonjwa asitembee kwani atasambaza sumu mwilini yaani abebwe palepale.
  • usifunge kamba kwenye mguu kwani imeonekana haizuii chochote zaidi ya kuharibu kiungo husika.
  • usichanje na wembe au kunyonya na kutema sumu kwani utaharibu mishipa ya damu
  • usiweke barafu kwani hakuanushahidi kwamba inasaidia.
  • piga simu kuomba msaada ili mgonjwa apelekwe hospitali.
  • usiweke pombe kwani huongeza ukubwa wa mishipa ya damu na kusambaza sumu zaidi.
  • kama nyoka amekufa nenda naye hospitali daktari amuone ili ajue kama ana sumu au hana sumu.

matibabu ya hospitalini..
kulingana na hali ya mgonjwa hupewa vifuatavyo…

  • huongezewa maji mwilini, hii husaidi kuongeza presha ya damu na kupunguza sumu.
  • hupewa dawa za kuua bacteria[antibiotics]
  • huchomwa sindano ya tetenasi
  • hupewa dawa za maumivu.
  • hushauriwa asiwe na wasiwaasi.
  • kidonda huoshwa na maji mengi na kuondoa jino la nyoka kama lipo.
  • mgonjwa atapewa dawa ya kuondoa sumu mwilini kama ikithibitika nyoka alikua na sumu ambayo inaitwa kitaalamu kama polyvalent antisera kama nyoka hana sumu mgonjwa hatapewa dawa hii.
  • dawa ya kuondoa sumu  hutakiwa utolewe ndani ya dakika 20 kama sio hivyo mgonjwa atafariki.

Story By:@Joplus_

Source:Muungwana Blog