RUBY AFUNGUKA KWANINI HAKUTOA VIDEO YAKE.

Kuna uwezekano mkubwa video ya wimbo wa Forever wa Ruby isitoke tena. Muimbaji huyo ameitaja sababu ya kushindwa kuiachia kichupa cha wimbo huo.Akiongea na Bongo5, Ruby amesema kuwa idea zilizotolewa na watu kwenye shindano la kumtafuta model na director watakaoshiriki kutengeneza video hiyo ni moja ya sababu iliyomfanya ashindwe kufanya kazi hiyo.
“Video ya Forever sikuitoa kwa sababu niliona tayari nyimbo imesha-trend, not only that niliona mashabiki nilivyotoa lile shindano la kutafuta video queen na director walijitokeza watu wengi kwenye kuifanyia video,” amesema muimbaji huyo.
“So many ideas zilitokea kwahiyo nikaona ni kitu ambacho kimekubalika kwa mashabiki,” ameongeza.
Muimbaji huyo ameahidi kuachia ngoma kali na kufanya vizuri zaidi ya alivyowahi kufanya kwenye nyimbo zake alizowahi kuziachia.

Story by:@Joplus_

Source: Raha za walimwengu