TYGA KUKUMBANA NA KESI NYINGINE BAADA YA KUMPA ZAWADI MPENZI WAKE.

Kylie Jenner ameingia rasmi kwenye kesi za Tyga, kuhojiwa kuhusu zawadi alizopewa na Tyga.

Zawadi ambazo amekuwa kipewa mrembo huyo na Tyga zimezua maswali na watu wanaomdai Tyga wametaka Kylie ahojiwe kuhusiana na maisha ya kifahari ya mpenzi wake.

Mwanasheria wa Jason Arasheben aliyemfungulia Tyga mashitaka ya kumdai Dola 270,000 za vyeni vya thamani alivyokopa 2013, ameuambia mtandao wa  Entertainment Tonight kuwa mahakama imeamuru wawili hao wajisalimishe wenyewe kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya Oktoba 6, wote watahojiwa ila tofauti.

 “We will ask him questions related to his finances, such as to his source of income to support his lifestyle as well as to pay for the extravagant gifts he buys Ms. Jenner, He will have to answer under oath and so will Ms. Jenner.”

Tyga kila kukicha amekuwa akiandamwa na kesi za madeni lakini bado ameendelea kuishi maisha ya fahari ikiwemo kumzawadia mpenzi wake, Kylie magari ya bei ghali na mengine mengi.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com