Tarehe 18 mwezi wa 7 Petitman Wakuache aliingia kwenye headlines za Perfect255 kwa kufunguka kuwa ameondoka rasmi katika kampuni ya Endless Fame ya mwanadada Wema Sepetu na hivi sasa yuko anasimama yeye kama yeye na wasanii wake Billnass na Nuh Mziwanda.
Sasa hiyo sio kesi, kesi ni kwamba Nuh Mziwanda amesikika akikanusha kauli ya hiyo ya Petitman na kudai kuwa petitman hajawahi kuwa meneja wake bali walikuwa wanafanya kazi kishkaji tu.
Akiongea na Enews ya EATV Nuh Mziwanda amedai kuwa Petit hakuwa na sifa za kumsimamia yeye kama msanii mkubwa, kwasababu Petit amemkuta yeye anajina tayari na pia kuna vitu vingine ambavyo ameona kwamba Petit hawezi kumtimizia yeye kama msanii. Na hivyo amesisitiza kuwa kwasasa yeye yuko chini ya Mchafu Chakoma wanafanya kazi na anamsaidia kama Brother.
“Inabidi ionekane tofauti kipindi niko na management na kipindi sina managemant, kipindi tunaanza kazi na petit yeye kanikuta tayari nina jina, nimepigana kimpango wangu hadi kuwa Nuh. Awali niliamua tu tufanye kazi kwasababu yeye ni kijana mwenzangu na wote tunatafuta, lakini kama manager unatakiwa kujua ni kitu gani unamfanyia msanii wako ili azidi kujibrand zaidi aweze kupiga mtonyo, lakini kuna vitu me nahisi Petit alikuwa anashindwa kuvitekeleza kwangu mimi ili twende sawa. ndipo me nilipoona kwamba nimeshafeli kwa miaka 3 kwasababu ya mapenzi na nikashuka kimuziki,kwahiyo sitakuwa tayari nifelishwe tena na mshkaji tu ambaye sio hata mpenzi wangu., ambaye kaja tu kanikuta mimi nina jina langu tayari.” Alisema Nuh Mziwanda
Alidai kuwa hawezi kuviongea vitu ambavyo Petit alishindwa kuvitekeleza kwake na badala yake aliongeza kuwa kwasasa hataki tena kufeli kama alivyofeli mwanzo.
“Sipo tena na Petitman na sasa hivi nipo na mchafu kama Brother ambaye ananisapoti sio kusema kwamba tumemwaga wino namuheshimu kwasababu anapenda maendeleo yangu.” Aliongeza Mziwanda.
Story by:@Joplus_
Source: Perfect255.com