SAIDA KAROLI: DIAMOND KAUTENDEA HAKI WIMBO WA “SALOME” NA NINA IMANI NAYE KATIKA TASNIA HII YA MUZIKI.

Baada ya Diamond Platnumz kuachia ngoma ya “Salome” ambayo imetokana na ngoma ya “Maria Salome”, Sasa Saida Karoli ameanza kuwa na matumaini na Diamond.

Saida Kalori msanii wa loong tyme veteran wa muziki wa asili na hivi karibuni Diamond platnumz ame release remix ya ngoma ya Saida inayoitwa Maria Salome na ya Diamond inaitwa Salome, Sasa OG ya ngoma hii ilitoka miaka ya mwanzoni mwa 2000, Perfect255 ikaamua kumsogezea nyaya Saida Karoli ili kubonga naye.

Akiongea na Perfect255, Saida Kalori amefunguka kwamba huu wimbo wa “Salome” umekaa sawa na upo vizuri na anamatumaini kwamba sasa hivi kazi zetu watanzania zitaanza kufanya vizuri kila kona ya Dunia.

Perfect255 haikuishia hapo katika kupiga stori na Saida Kalori, Perfect255 ikatamani kujua vibunda vya mtonyo ambao ameupokea Saida kutokana na ngoma hiyo, Lakini good newz ni kwamba Saida Kalori alisema kwamba pesa sio kitu, kitu cha muhimu ni utu kwasababu utu ndio unathamani kubwa kwasababu anamiini kwamba wimbo huo utakuja kuingiza pesa nyingi lakini utu utakuwa daima.

Mwisho kabisa tutegemee kumwona upya Saida Kalori kwani tangu wimbo huu wa “Salome” utoke Saida ameshapokea deals kibao kutoka kwa makampuni tofautitofauti.

Story By:@Joplus_

Source:Perfect255.com