Emmy Awards ni tuzo zinazotolewa kwa mastaa wa filamu kila mwaka, Na ninafahamu kuna watu wangu ni wapenzi kufatilia tuzo kama hizi za mastaa wa filamu mbalimbali za nje.
Usiku wa September 18 2016 zimetolewa tuzo za 68 za Emmy ndani ya Microsoft Theater, Downtown Los Angeles Marekani ambazo zimeshikilia headlines kwenye mitandao mbalimbali ambapo pia staa mmiliki wa album ya ‘Lemonade‘  Beyonce Knowles alitakiwa kutoa suprise perfomance usiku wa tuzo hizo.
Imeripotiwa na kituo kikubwa cha habari za mastaa, Enews cha marekani kuwa staa huyo alitamani kuwepo katika tuzo hizo lakini hakuwa vizuri kiafya na kumfanya ashindwe kufika kwenye tuzo hizo.
Story By:@Joplus_
Source: Millard Ayo