BEN POL AWEKA WAZI MIPANGO YAKE BAADA YA MOYO MASHINE.

Moyo Mashine ni ngoma ambayo imefanya vizuri sana kiasi kwamba hata mmiliki wa ngoma hiyo Benpol hakuwa na imani kama ngoma hiyo inaweza kufikia mafanikio hayo.

Video ya ngma hiyo imefikisha zaidi ya viewers 1,378,000 hadi sasa, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika ngoma nyingine yoyote ya Benpol. Hiyo inadhihirisha kuwa huenda Moyo Mashine ndio ikawa ngoma bora kabisa kuliko ngoma zote za Benpol.

Perfect255 imepiga story na Benpol kutaka kujua ni mipango gani anayo kuhusu kazi baada ya ngoma hiyo ya Moyo Mashine kufanya poa.

“Kazi zipo nyingi, nimefanya kazi na wasanii kibao wa nje na mwezi Desember natarajia kusafiri kwenda Europe kushoot video ya ngoma yangu nyingine lakini jina nimeliweka kapuni.” Alisema Benpol.

Chidinma wa Nigeria ni mmoja kati ya wasanii ambao wametajwa kwenye list ya wasanii wa nje ambao Benpol amekwisha fanya nao kazi. List nyingine unaweza kuisikiliza hapa chini kwenye hii video ambayo ina full interview ambayo Benpol amefanya na Perfect255.

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com