SABABU YA ROMA KUSHUSHWA KWENYE STAGE YA FIESTA 2016 MOROGORO.

Jumapili ya septemba 18 ilikuwa ndio siku rasmi ya kihistoria kwa mvua ya burudani kuwanyeshea wakazi wa Morogoro katika msimu huu wa Fiesta.

Ni wasanii wengi na wakali ambao walikuwa wamepangwa kufanya show usiku huo bila kumsahau Staminah ambaye alikuwa mwenyeji usiku huo.

Ilikuwa ni time ya Staminah kufanya show ndipo Rhymes of Magic Attraction (R.O.M.A) alipo panda jukwaani kama surprise kutaka kumpa nguvu Staminah na kuperform ngoma yao ya “Mmeniroga remix” ambayo wamefanya wawili hao pamoja na mkongwe Jay Moe.

Ndipo mzuka ulipompanda Roma hadi kushindwa kujizuia na kujikuta anatoa lugha chafu akiwa jukwaani hapo na kusababisha show hiyo kushindwa kuendelea huku akishushwa kutoka jukwaani na ma-bodyguards na kuondolewa kabisa katika show hiyo.

Roma aliambatana na Mke pamoja na Mtoto wake katika show hiyo, kitu ambacho kilimpa wakati mgumu sana Mke wake baada ya tukio hilo kutokea na kujikuta akibwaga machozi bila kujua ni nini kinaendelea.

Soudy Brown amemtafuta Roma na kupiga nae story kuhusu tukio hilo, yapo mengi ya kusikia kutoka kwake. Itazame hii video hapa chini ili kujua alicho kizungumza Roma.

Story By: @Joplus_

Source: Perfect255.com