FAHAMU UNDANI WA TALAKA YA ANGELINA JOLIE NA BRAD PITT.

September 19, 2016 kituo cha TV cha CNN kiliripoti kuhusu muigizaji mwenye mvuto wa kipekee kuanzia muonekano wake mpaka uigizaji wake, Angelina Jolie kufungua kesi ya kudai talaka kutoka kwa mume wake Brad Pitt, sababu zikilielezwa kuwa ni ndoa yao kukosa maelewano mazuri.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, wapenzi hawa walitengana kuanzia September 15, 2016, ikiwa ni miaka miwili na mwezi mmoja tangu walipofunga ndoa yao mnamo August 2014. imeelezwa kuwa Jolie anatafuta makazi mapya kwaajili ya kuishi na watoto wao sita huku akiiomba mahakama kumpa ruhusa Brad Pitt kuwatembelea watoto wake.
Inadaiwa pia Jolie ameiomba mahakama kumpa mamlaka ya kubakia na mali zote walizipata kwenye ndoa yao na suala la kugawana lifanyike siku za baadaye sana, ingawa pande zote mbili pia zimekubaliana kuhakikisha kuachana kwao kunakuwa kwa amani kabisa
>>>Ninahuzunishwa sana jambo hili, lakini kitu cha muhimu kwasasa ni usalama wa watoto wetu, nawaomba waandishi wa habari muwape uhuru kidogo watoto hawa kwenye wakati huu mgumu kwetu. Brad Pitt ameiambia CNN.
Akiongea na E! News jana Jumanne, Geyer Kosinski ambaye ni Meneja wa Jolie amesema kuwa Angelina yuko tayari kufanya jambo lolote ili kuwalinda watoto wake.

Ikumbukwe kuwa Pitt na Jolie walifunga ndoa yao mwaka 2014, lakini uhusiano wao ulianza rasmi waka 2004, baada tu ya kushiriki kwenye filamu ya “Mr. & Mrs. Smith.” wakati hupo, Brad Pitt alikuwa kwenye ndoa na muigizaji Jennifer Aniston. Mnamo January 2005, Pitt na Aniston walitangaza kuachana baada ya Aniston kufungua kesi ya kudai talaka ikiwa ni miezi michache baada ya ishu za Jolie kuanza kujitokeza.
Jolie na Pitt wana jumla ya watoto 6 ambapo watatu kati yao ni watoto wa kuwaasili kutoka nchi za Kenya, Ethiopia na Vietnam.
Angelina Jolie ni balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya wakimbizi, moja kati ya ishu kubwa zinazojadiliwa kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulioanza September 19,  2016 huko New York Marekani.
Story By:@Joplus_
Source: Millard Ayo