AVRIL ASHTUA HISIA ZA RAYVAN WA WCB.

Raymond ameamua kuusemea moyo wake mbele ya mashabiki maelfu kwenye show ya WCB, Mombasa, Kenya.

Muimbaji huyo wa ‘Kwetu’ alimpandisha jukwaani mrembo wa Kenya, Avril na kumuimbia wimbo maalum kuelezea hisia zake waziwazi kuwa ni msichana anayempenda na kuwaacha mashabiki wakiangusha shangwe za kutosha.

Hakuuishia hapo, Ray alipost picha akiwa na Avril na kuandika:

Trust me @theavieway I really love you … thanks for coming … God bless you.”

Avril naye alionesha kudata kwelikweli na dogo huyo kwakuwa hakuisha kupost picha na video za show yake.

“This song that @rayvanny serenaded me with should be my next collabo hmmmm #ThinkingOutLoud,” aliandika kwenye picha aliyoweka Instagram akiwa na mkali huyo wa freestyle.


Hadi sasa tunafahamu kuwa Avril yupo single baada ya kuachana na mpenzi wake Msouth na pia Ray hajawahi kuonesha kuwa na msichana yeyote na hivyo wawili hawa wanaweza kuwa ‘perfect combo.’

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Raymond, Harmonize na Rich Mavoko walikuwa na show kwenye  mwambao wa Mombasa nchini Kenya.

Reporter:@joplus_
Source: Udaku Special Blog