Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameamua kufunga uwepo wake kwenye video za wasanii wa Bongofleva unaimpact kubwa
Hivi karibuni mwanadada Shilole ameusika sana kwenye video kibao mpya za mastaa wa bongo, kama “Inde” ya Dully Sykes, Raymond “Natafuta Kiki”, Man Fongo Hainaga ushemeji na video kibao, shilole ameongea hayo kupitia kipindi cha EA TV kwa kusema kwamba uwepo wake kwenye video za wasanii unaleta impact kwa watu kwa kuwa wataitzama sana video hiyo.
“Nilifanya video ya Man Fongo haina ushemeji, video ya Darasa ‘Too much’ hii ya Raymond ‘Natafuta kiki’ na ile ya Dully Skyes na Harmonize ‘Inde’ wao wamekuwa wakiniomba na kusema uwepo wangu kwenye video zao unaleta ‘impact’ kwa watu kwani watu wanakuwa wanazitazama sana video zao hivyo mimi naamua kuwapa ‘support’
Story By:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.