Siku zote ukiwa unafanya kazi zako vizuri na mafanikio yakiwa yanakuja lazima pia kuna kitu kizuri utakuwa unakiandaa, Young Thug kaamua kununua mjengo wake mpya baada ya mafanikio kibao aliyoyapata.
Young Thug ni moja ya maartist ambao kwa mwaka huu amejitahidi kufanya vizuri baada ya kuachia project yake ya “Jeffery” ambayo kwa mara ya kwanza ilizua mijadala ya maneno kuwa anabadilisha jina lake, vilevile cover album ya “Jeffery” nayo ilileta gumzo kwa kusemwa amevalia nguo za kike, ila all in all album ya “Jeffery” ni album ambayo imevunja rekodi ya chati za Billboard kwa kuingia katika top 5 ya Top Rap Albums chart 2016.
Mafanikio mengine makubwa ni pale katika wiki ya kwanza ya project yake ya “Jeffery” iliuza kopi 37,000 na kufanya pia kushika nafasi ya nane katika chati za Billboard.
Kikubwa kabisa Young Thug anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Jerrika Karlae.
Story By:@Joplus_
Source:Perfect255.com