ALI KIBA AWEKA WAZI UKWELI WA JINA “KING KIBA”

Alikiba ametoa ufafanuzi wa wapi #KingKiba ilitokea kiasi cha kuitumia katika sehemu nyingi.
Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz kilichoruka Alhamis hii kupitia EATV, Kiba alisema ni mashabiki ndio waliombatiza.
“Wakati nimepumzika kwenye muziki kulikuwa kuna vitu vingi vinavyoendelea, kuna watu walikuwa wanaongea kwenye social media. Kuna watu walikuwa wananifikia sababu wanapajua nyumbani wakasema ‘au tuanzishe kampeni’ wakaanzisha mimi najua masihara,” alisema.
“Kiukweli walichokuwa wanacomplain, kwanini Ali hutoi nyimbo, uko wapi, kuna watu wakaanzisha Bring Back Our Alikiba. Ndio ikaanzia pale watu wakaanza kuniita King Kiba kwasababu hata kwenye show pale wakawa wananiita hivyo,” aliongeza.
“Nikaona sawa haina shida, kila kitu ikawa hashtag #KingKiba, lakini sikufikiria kujiita hivyo.”
Kwa upande mwingine muimbaji huyo wa Aje alisema kuwa kutomfollow mtu yeyote Instagram haimaanishi kuwa anaringa.“Nimeacha kufollow watu [Instagram] nikiwa na watu 50k,” alieleza.
“Nilikuwa nataka nione, nimekuja kwenye muziki, je nina fans wangapi watanifollow mimi nikiwa kama AliKiba na kuangalia kazi zangu. Nilikuwa nasikia watu wanasema naringa na nini, lakini nilisema kwamba nitawafollow watu baadaye.”

Story By:@Joplus_

Source: Raha za walimwengu