COLABO YA DIAMOND NA RAYVAN “SALOME” ILIPATA BARAKA KUTOKA KWA FELICIAN MUTAKYAWA.

 Leo imedropishwa hitsong kutoka katika lebo ya WCB, Hit ambayo imevikutanisha vichwa viwili kutoka katika Lebo hiyo.

Ni Raymond (Rayvanny) na Diamond Platnumz ndio ambao wame-take over leo kwa ngoma yao ya “Salome”

Kama ni mkongwe kidogo na ulikuwa msikilizaji na mpenzi wa muziki kwa miaka ya 2000 naamini kabisa utakuwa umeifananisha ngoma hii ya Salome na ngoma ya Maria Salome ya mwanamama Saida Karoli.

Japo sio kwa mashairi, ila melody na title ya nyimbo ni wazi kabisa kuwa ngoma ya Maria Salome imehusika humo ndani.

Kama ulikuwa unataka kuvitumia vigezo hivyo kama diss basi jua kabisa umefeli kwasababu WCB sio watu wa mchezo mchezo.

Unachotakiwa kukijua ni kwamba wakali hao waliutafuta uongozi wa Saida Karoli na kuuomba vibali na baraka zote juu ya ngoma hiyo, na Sallam S.K ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz ametuthibitishia hilo baada ya kupost katika ukurasa wake wa instagram picha ambayo iliwaonyesha Diamond na Raymond wakiwa kwa Mzee Felician Mutakyawa ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa mwanamama Saida karoli.

Kama hujapata bahati ya kuisikia ngoma hiyo mpya ya Diamond na Rayvanny sikiliza hapa

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com