CHAMBUA KAMA KARANGA YA SAIDA KAROLI ILIWAHI KUTUMIKA KWENYE MOVIE HOLLYWOOD.

Diamond ameachia wimbo mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Ray vanny, wimbo huu umechukua vionjo kwa asilimia kubwa kutoka kwenye wimbo wa ‘Chambua kama karanga/ Maria Salome’ wa Saidi Karoli.

Tumeona tukukumbushe mambo ambayo labda hufahamu kuhusu wimbo wa ‘Chambua kama karanga’ wa Saida Karoli. Mbali ya kuwa wimbo huo ulitoka kipindi cha mwaka 2000 mwaka 2013 ulitumika kwenye filamu ya Marekani ya muongozaji maarufu Tyler Perry ‘Peeples’

Filamu hiyo imeigizwa na mastaa kama Kerry Washington, Craig Robinson na Malcolm Barrett.

Hatahivyo Saida Karoli alidai kuwa hakupokea malipo yoyote kutoka kwa waandaji wa filamu hiyo japo alisema arifurahi kuona kazi yake imepewa heshima ya kutumika kwenye filamu hiyo.

Wimbo huo pia ulibeba jina la Albam ya kwanza ya saida karoli iliyozinduliwa tarehe 2 Septemba mwaka 2001,  ‘Maria Salome’ ni moja ya album za muziki za Tanzania zilifanya vizuri zaidi sokoni.

Mwaka 2012 Saida Karoli alikua msanii pekee wa kike kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo za KORA, alikuwa anawania kipengele cha ‘Mwanamuziki bora wa kike wa Afrika Mashariki’.

Story by:@Joplus_

Source:Perfect255.com