TEAM YA FIESTA YAFANYA ZIARA SHULE YA USAGARA SECONDARY ILIYOPO TANGA KABLA YA KUTOA BURUDANI USIKU WA LEO.

Leo ndio siku ambayo historia ya burudani inaandikwa mjini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

Ni ule msimu wa Fiesta na leo ni zamu ya Tanga. Asubuhi ya leo team nzima ya Fiesta ilienda kuitembelea shule ya Secondary ya Usagara, shule ambayo msanii wa Hiphop Tanzania Roma Mkatoliki alisoma hapo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Ikiwa dhumuni la ziara yao ni kutoa somo kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwapa michongo ni jinsi gani wataweza kutimiza ndoto zao kupitia elimu.

Instagram photo by Clouds Fm_BKsYdXwA0gG - JPG
Msanii Roma Mkatoliki akitoa Somo kwa Wanafunzi wa Usagara Secondary
Instagram photo by Clouds Fm_BKsaJEnApuH - JPG
Snura akibonga na wanafunzi wa Usagara Secondary
Instagram photo by Clouds Fm_BKsYqkQg4Yv - JPG
Picha ya Wasanii wakiwa katika moja ya darasa la shule hiyo

Instagram photo by Clouds TV_BKsZIDqDwTA - JPG

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com