Kiwanda cha muziki barani Afrika kimepata pigo baada ya Star wa muziki wa Kwaito kutoka Afrika Kusini, Mduduzi Edmund Tshabalala a.k.a Mandoza kufariki dunia mapema jana September 18 baada ya kuugua ugonjwa Kansa iliyomsumbua kwa zaidi ya miaka miwili, na iliripotiwa kuwa ilikua imeanza kusambaa kwenye ubongo wake, na kumfanya apoteze uwezo wa kuona kabisa.
Tweets za taarifa ya kifo chake kutoka vyombo vya habari vya Afrika kusini na mastaa mbalimbali zimeonesha kuguswa na msiba wa msanii Mandoza…. RIP.
kifo cha Mandoza kimetokea siku tisa baada ya msanii huyo kufanya show yake ya mwisho kabla ya mauti kumkuta, nimekuwekea hapa video mtu wangu.