SALOME YA DIAMOND PLATNUMZ NA RAYVAN YAFICHUA MENGI.


Wengi tunajua kwamba wimbo wa “Salome” wa Diamond ni wimbo ambao umetoka katika ngoma ya“Maria salome” sasa je Saida karoli amepata shavu la mtonyo?Diamond Platnumz Weekend hii ameachia ngoma inaitwa Salome amemshirikisha Rayvanny, na ndani ya wimbo huo wa “Salome” diamond amerudia melody ya ngoma ya “Maria salome” kutoka kwa legendarySaida Karoli, ngoma ambayo ilikuwepo kwenye album ya mwaka 2001 karibu miaka 16 iliyopita.Sasa Diamond amerudia vitu flani flani hivi ambavyo sio mbaya kumuenzi Bi Dada kwasababu sheria za kimataifa za Hati miliki zinasema kwamba kurudia ngoma ya msanii fulani bila kuulizwa ni mpaka ngoma iwe imefikisha miaka 50 sasa kwa Diamond ilikuwaje?
Akiongea na Pe Diamond amefunguka na kusema kwamba siku tatu nyuma Diamond alishafanya mazungumzo na uongozi wa Saida Karoli kwasababu Diamond yeye kama yeye anasema kwamba anaheshimu kazi ya mtu na hapendi mtu kazi yake aichukulie kwa dharau na vilevile kuna kiasi cha hela ambacho Diamond alikitoa na kutoa share kwake kwamba kila amount ya pesa inayoingia kwenye video hiyo basi Saida naye atakuwa na share yake.
Kingine pia ambacho ulikuwa ukifahamu kuhusiana na wimbo huu wa Salome ni kwamba siku ambayo timu ya WCB ilipoalikwa kupata chakula cha mchana kwa Mh Jakaya Mrisho Kikwete, Diamond alimwoneshaMh Jakaya Mrisho Kikwete hiyo video ya Salome na akatokea kuikubali sana.
Story By:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.