Baada ya mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya wimbo ‘Inde’, Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.
Hivi karibuni Nuh alidai katika maktaba yake ana wimbo ambao unaitwa ‘Inde’ lakini atashindwa kuutoa baada ya kusikia ‘Inde’ ya Dully mtaani huku akimtuhumu producer wake kula njama na Dully Sykes na kutoa idea ya wimbo huo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Dully Sykes amesema idea ya wimbo ‘Inde’ haikuwa yake, alipewa na Harmonize na yeye kuiboresha zaidi.
“Idea ya ‘Inde’ siyo yangu,” alisema Dully Sykes. “idea ya ‘Inde’ niya Harmonize, nimemkuta nayo mimi nilikuwa sina hata idea hiyo yakusema niimbe ‘Inde’, wala sijui kuhusu maswala ya Inde,”
Alivyoulizwa Harmonize kuhusu idea ya wimbo ‘Inde’ alisema, “Labda mimi nizungumze kitu kimoja, unajua mimi ni msanii mchanga sana, kwanza sina hata miaka 3, siyo kwamba najua sana vitu vingi, lakini vichache navyovijua huwa napenda sana kuweka wazi ili na watu wavijue. Unajua mtu kama Dully Sykes mimi nimeanza kumsikia toka nipo kijijini huko, kila siku anatoa nyimbo, ana hit kibao.
Sometime vijana tukiwa tunatafuta angle tutafute angle nzuri kwa sababu kuja kumwambia brother Dully kachua wimbo wako au kaiba, unamvunjia heshima, unaukosea heshima muziki wa bongofleva pia, kwa sababu unavyomzungumzia brother Dully unauzungumzia muziki wa bongofleva, so kumwambia brother Dully wimbo uliotoa na mimi na wimbo wangu wa miaka miwili sijautoa ni kumkosea heshima,” alisema Harmonize.
Wimbo ‘Inde’ wa Dully Sykes unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na rudinga huku YouTube ukiwa na views milioni moja kwa kipindi cha mwezi mmoja toka utoke.
Story by:@Joplus_
Source:Muungwana Blog