KOLABO YA WEUSI NA SAUTI SOUL YATEGEMEWA KUACHIWA HIVI KARIBUNI.

Ule wimbo wa Weusi na Sauti Sol ambao umefanyika nchini Kenya siku chache zilizopita unaweza ukasikika kabla ya mwaka huu kumalizika.

Japo siku chache zilizopita alipoongea na Bongo5, Joh Makini alishindwa kuweka wazi siku ambayo wimbo huo utatoka lakini kupitia akaunti ya Instagram ya mmoja kati ya member wa kundi la Weusi, G-Nako ameweka picha wakiwa na wasanii wa kundi la Sauti Sol na ameandika ujumbe ambao unaweza ukawa unathibitisha kuwa wimbo huo utatoka kabla ya mwaka huu kuisha.
“(E.A) WATU WA MUNGU IMESHAIVAA TAYARI NA MWAKA HAUISHII INAKUJA INSHALAAH!! ,” ameandika G-Nako kwenye mtandao huo.
Muda utaongea na tutajua kama ujumbe huo ulikuwa unatufahamisha kuhusu ujio wa wimbo huo au ni tofauti.
Story by:@Joplus_
Source: Muungwana Blog