DIAMOND AMPIGIA DEBE ALIKIBA KWA MASHABIKI ZAKE WAMPIGIE KURA KTV EMA AWARDS 2016.

Mondi Bin Awards Diamond Platnumz amewataka mashabiki zake wampigie kura msanii Alikiba kwenye tuzo za MTV EMA akiwa kama msanii pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo.

Licha ya tofauti ambazo inasemekana wawili hao wanazo, mkali huyo amewataka mashabiki wake waweke mambo ya u-team pembeni na wajikite kwenye kuliletea taifa faida.

Akihojiwa kwenye kipindi cha D’Wikend Chatshow kinachoruka Cluds TV Ijumaa saa 3 usiku Diamond Platnumz alidai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Alikiba ndio maana habari za tofauti zao zinazidi kupungua siku hadi siku, na kama angekuwa na tatizo nae kweli basi ingejulikana wazi kwasababu yeye bifu lake huwa haliishi na wala sio la kujificha.

Inatia hamasa na kuona ni jinsi gani wasanii wetu wanatumia nguvu nyingi kuweza kuufikisha muziki wetu sehemu fulani ambayo italipa heshima taifa letu pia. Unaweza kutoa maoni yako kuhusu kitendo hiki cha Diamond Platnumz, tuachie hapa chini kwenye uwanja wa comments.

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com