TIMBWILI LA UWOYA NA MASOGANGE KANISANI

Akina dada wenye ‘taito’ kubwa Bongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ na Agnes Gerald ‘Masogange’, wanadaiwa kuzua kizaazaa cha aina yake baada ya hivi karibuni kutinga kwenye Kanisa la Christ Embassy lililopo Mbezi-Makonde jijini Dar kwa nia ya kumrudia Mungu wao. Chanzo makini ambacho ni miongoni mwa wasanii wanaoabubu katika kanisa hilo kilichoomba hifadhi ya jina gazetini kilidai kuwa, mara ya kwanza mastaa hao kufika kanisani hapo, baadhi ya waumini wanaowafahamu walishindwa kuamini kama kweli wameamua kubadilika au walikuwa na lao jambo hivyo kusababisha minong’ono iliyowafikia waumini wengine waliokuwa hawawajui, nao kuanza kuwashangaa. 

“Unaambiwa siku hiyo tulipofika pale kanisani, achilia mbali sisi, watu walioibua mshangao sana ni Irene ambaye ni staa wa sinema za Kibongo na Masogange ambaye ni video queen wa Bongo, maana pale walipokuwa wamekaa watu walikuwa wakipishana kuwashangaa na wengine kutaka kupiga nao ‘selfie’.
“Kiukweli katika siku za mwanzo mastaa hao walikuwa ni gumzo, walipokuwa nje walikuwa wakizongwazongwa na watu, yaani ibada ilipoanza ndipo walipokuwa na amani,” alidai mtoa habari huyo. Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hali ilikuwa hivyo katika siku za mwanzo lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, waumini hao wakawa wamewazoea na kuamini kuwa ni kweli wameamua kumrudia Mungu baada ya kukaa huko walikokuwa kwa muda mrefu. 
SKENDO ZAO NDIYO CHANZO Ilielezwa kwamba, kuibua kwao kizaazaa kanisani hapo kulitokana na namna ambavyo wamekuwa wakiandikwa kwenye magazeti kwa skendo mbalimbali hivyo walipoonekana kwenye eneo hilo takatifu waliwashangaza wengi.
 “Unajua mastaa hawa wameandikwa sana, hivi ni skendo gani ambayo hawajawahi kuikanyaga? Sasa kitendo cha wao kuonekana pale kiliwafanya wengi washindwe kuamini macho yao. “Kuna muda ilizuka mijadala ya vikundi kuwajadili wao lakini wengi waliishia kusema kuwa Mungu ametenda kwa kuwafanya mabinti hao kuamua kuokoka,” alizidi kudokeza sosi wetu huyo. 
 
KUMBE SIYO WAO TU 
Hata hivyo, ilidadavuliwa kuwa, siyo mastaa hao tu wanaofika kwenye kanisa hilo bali pia wapo Mary Mawingi, Lisa Jensen, Chopa Mchopanga na wengineo.
Uwoya: “Kama ni kwenda kuabudu kila Jumapili huwa nakwenda kama Mkristo mwingine. Kuokoka siyo kusali kanisa la kilokole bali ni kumpokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yangu na mimi nilishafanya hivyo tangu nikiwa mdogo kwa mama yangu, hayo ya kuzua kizazaa siyajui kwani naona ni kawaida tu watu kunishangaa.” Masogange: “Jamani siku hizi sipendi kabisa mambo ya kuandikwa magazetini, sitaki kufuatiliwa maisha yangu.” Mary Mawigi: “Lile kanisa ni la kipekee, kuacha kwenda siyo rahisi kwani pale tunajifunza mambo mengi! Tangu nimeanza kusali pale najiona ni mpya.”@Joplus_
Source: www.rahatupu.us