IGGY:SINA MPENZI KWA SASA,MIMI NA FRENCH MONTANA NI RAFIKI TU.

 Tujikumbushe..

Ex wa Iggy ambaye ni mcheza kikapu maarufu Marekani aliwahi kuwa ambia mtandao wa TMZ kuwa atafurahi kuwaona wawili hao wakiwa pamoja na hata kufunga ndoa “No man, I’m happy for them. I wish they’d get married, ” alisema Nick.

Hii ilitokea baada ya picha zao kusambaa mitandaoni. Iggy amekuwa na Montana kwa zaidi ya
mwezi mmoja sasa.

Mchongo huu hapa..

Iggy Azalea amekataa kuwa na uhusiano na French Montana japo wameonekana mara kadhaa wakiwa sehemu za starehe pamoja.Rapper huyo wa kike ameuambia mtandao wa TMZ kuwa hana mpenzi kwa sasa hivyo yeye na French Montana ni marafiki tu.

“We are Single, I’m single,” amesema Iggy.“just friends.”

Wiki kadhaa zilizopita Iggy alidai kuwa yeye na French Montana kuna wimbo wamefanya ila hawana mahusiano yoyote lakini baada ya wiki moja wawili hao walionekana wakiwa wanakula bata pamoja huko Cabo San Lucas, Mexico. Walionekana pia wakibusiana.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com