STEVE RNB:WATU BADO HAWAJUI MUZIKI WA KUPERFORM LIVE.

Steve RnB ambaye huwa anafanya show zake live amesema hili ni kutokana na wasanii kutoelewa maana ya muziki kwa ujumla wake lakini pia pengine hatujafikia muda wake kuelewa.
Kupitia PB steve amekaririwa akisema ubora wa muziki wa live ni tofauti na kufanya playback na hata nyimbo zilizorekodiwa live zina vitu ambavyo huwezi kuvipata endapo utarekodi kwa mtindo wa kawaida.

Baadhi ya nyimbo za bongofleva zilizorekodiwa live ni KamaZamani ya Mwana Fa, Mwana ya Alikiba, keepYouWarm ya Hisia n.k.
Kwa kuangalia clips za video wanazoweka mitandaoni utaona upungufu mkubwa wa uwezo wao (wasanii wakibongo)wa sauti pindi Dj anapo-mute sauti ya wimbo ili msanii asikike.
Hata hivyo wengi wamekuwa wakisema Gharama za kufanya show na live ndicho chanzo cha wao kufanya hivyo.
Wapo wasanii wanaojitahidi kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuperform na Cd yenye beat tupu na hivyo kusaidia kuwa na ladha tofauti jukwaani.

Story by:@Joplus_

Source:Raha za walimwengu.