CHURA YA SNURA YAPEWA KIBALI REDIONI NA KWENYE TV.

Leo october 5 2016 Mrembo kutoka Bongoflevani Snura ambaye alizichukua headline baada ya wimbo wake wa Chura kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzani (BASATA) leo mtu wangu nina goodnews kutoka kwa Snura ni baada ya wimbo wake wa chura kuruhusiwa kuchezwa kwenye radio na TV baada ya kuruhusiwa

Snura amekutana leo na waandishi wa Habari na kuyasema mashariti ambayo ameyafata ili wimbo wake wa chura kupewa ruksa na Wizara ‘Leo nimewaita hapa kwasababu ya wimbo wangu wa chura kufunguliwa tena baada ya Serikali kuufungia tarehe  may 3 2016’>>>Snura

‘Hii ni baada ya kukukata rufaa na kukubaliana na Wizara kutengeneza Video nyingine ya wimbo wa Chura, baada ya kutengeneza video mpya ndio wimbo wangu wa Chura umefunguliwa na ni ruksa kupigwa kwenye TV na Radio nchini, pia namshukuru sana Waziri Nape’>>>Snura

Story by:@Joplus_

Source: Millard Ayo.