Ni ukweli usiopingika kuwa wasanii waliopo chini ya label ya muziki ya ‘WCB’ kwasasa ni moto wa kuotea mbali, na CEO wa label hiyo Diamond Platnumz yupo kwenye mipango ya kuongeza nguvu kwa kumsaini msanii wa nje ya Tanzania kwenye label hiyo.
‘Soon’ Diamond aliandika Twitter alipokuwa akijibu swali la shabiki yake lililomuuliza kama anampango wa kumsaini msanii wa nje ya Tanzania kwenye label yake.
Pia Diamond alisema ukiachana na collabo zake mwenyewe kuna collabo zingine za wasanii WCBÂ na wasanii wa nje.
Story by:@Joplus_
Source: Perfect255.com