UJIO MPYA WA FETTY KATIKA GAME YA UTANGAZAJI

Ilikuwa ni siku ya Jumanne ya September 15 mwaka wa 2015 ndio siku ambayo nyoyo za wapenzi wa burudani na hasa wale wapenda kusikiliza vituo vya redio ziliingiwa na huzuni flani hivi baada ya mwanadada ambaye ame wa-inspire wadada wengi wanaofanya kazi ya utangazaji kwa sasa Dj Fetty kutangaza rasmi kuwa anaachana na kazi hiyo.
Halikuwa jambo rahisi kwa wapenzi wa Clouds FM kuzoeana na hali ya kutokuwepo kwake katika kipindi cha XXL cha redio hiyo kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya ilikuwa nzuri tena yenye kuwavutia wengi.
Dj Fetty alitangaza kuachana na kazi hiyo na kudai kuwa anataka kujikita zaidi katika mambo ya biashara ambapo sasa anaendesha duka lake la nguo ambalo amelipa jina la Fettylicious Street look linalopatikana Dar Free Market.
Baada ya wasikilizaji na wadau mbalimbali kumuomba sana mwanadada huyo kurudi katika kazi yake ya awali ambayo ni utangazaji kutokana na kiu ya wasikilizaji hatimaye mwanadada Dj Fetty ameweka wazi huenda siku moja atarejea kufanya kazi hiyo ya utangazaji.
Akipiga story ameiambia kwamba endapo akirejea katika Clouds Media Group basi hatoweza kurudi katika kipindi cha XXL na badala yake ataenda kujiunga na kina Gadner G Habash,Ephraim Kibonde na George Bantu katika kipindi cha Jahazi.
Na Good news ni kwamba Gadner G Habash amelithibitisha hilo na kuahidi kwamba atahakikisha Dj fettyndio anakuwa mtangazaji wa kwanza kulipwa mkwanja mrefu zaidi ya wote Tanzania.@Joplus_
Tazama hii video hapa chini kulithibitisha hilo.Source: Raha za walimwengu