GIGY MONEY APIGILIA PINI TETESI ZA AMBER LULU KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA ARUSHA.

Mwanadada mrembo ambae amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa kutokea katika videos kadhaa za Bongo Fleva Amber Lulu inasemekana kwamba yuko chini ya usimamizi wa polisi kwa siku ya pili sasa.

Instagram photo by Amber___lulu_BLBOtMsjJnL - JPG

Ni kutokana na kinachosemekana kuwa amekamatwa na Sembe (Madawa ya kulevya) huko mkoani Arusha akiwa Airport akijiandaa kuyasafirisha hadi nchini China.

Taarifa zilimfikia Gossip Cop Soudy brown na akaona haitakuwa mbaya kama atapiga story na watu wa karibu wa mwanadada Amber Lulu ili kumpa ukweli juu ya suala hilo. Ndipo alipomvutia waya Gigy Money. Mapovu yaliyomtoka mwanadada Gigy sio ya polepole, na kudai kuwa kimbelembele cha mwanadada Amber Lulu ndio kimemfanya kupata matatizo.

Soudy Brown hakuishia kwa Gigy tu, alimvutia waya na rapper Young Dee ambaye kwa mujibu wa Gigy Money inasemekana kuwa ndiye boyfriend wa mwanadada Amber Lulu. Na Young Dee alikana kabisa kumjua mrembo huyo na akadai kuwa hajui chochote kinachoendelea kuhusiana na msichana huyo.

Ubuyu wote nimeukusanya hapa chini kwenye hii video unaweza kuitazama.

Story by:@Joplus_

Source:Perfect255.com