KAULI YA DAVIDO BAADA YA KUTOKUTAJWA KUWANIA TUZO ZA MTV MWAKA 2016.

September 23, 2016 jina la msanii Davido kutoka nchini Nigeria linazidi kuzungumzwa kila kona na safari hii sio kwa uzuri sana mtu wangu, maswali ni mengi juu ya ukimya wake kwenye kiwanda cha muziki. Hii imemfanya Davido kufunguka juu ya sababu za kupotea kwake.

Jina la Davido limekosekana kwenye vipengele vya tuzo nyingi zilizotolewa na kutajwa mwaka 2016, Ish hii imemfanya mmoja kati ya mashabiki wake kuandika kwenye Twitter juu ya nini kinachoendelea.

Kwa bahati nzuri, Davido alimjibu shabiki wake na kukiri kuwa hastahili kuwepo kwenye list ya washindi au wanaowania tuzo mbalimbali kwa mwaka 2016.

Mara ya mwisho kwa msanii Davido kuachia kazi zake ilikuwa ni miezi 11 iliyopita, na ilikua single ya ‘The Money’ aliyompa collabo Olamide na ilitoka November 7, 2015.

Story By:@Joplus_

Source:Millard Ayo.