TIMBULO AWAPA DONGO VANESSA MDEE NA MALAIKA BAADA YA KUTOSWA.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Timbulo
amefunguka na kusema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wamezoea kupata kidogo katika
maisha yao ya kila siku ndiyo maana inapotokea wamepata kikubwa wanawehuka na kuvurugika.

Timbulo alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz, akidai kuwa kuna baadhi ya wanawake wakipata fedha au mafanikio katika maisha yao wanabadilika na kuwa na mashauzi na kwamba wanajisahau walipotoka na kuanza kuonesha dharau.

“Watoto wa kike wamezoea kupata kidogo
wakipata kikubwa wanawehuka, wanabadilika
wanajiona wasichana wazuri.

“Na ikishatokea akaanza kuonekana kwenye TV vichwa vyao vina vurugika akili, wanashindwa kutambua nafasi walizopata, mimi naamini ukipata nafasi ya kufanya kazi na msanii yoyote anayefanya vizuri
ni nafasi nzuri kwa msanii wa kike na yeye kufanya vizuri” alisema Timbulo.

Msanii Timbulo alisema haya baada ya
kuzinguliwa na msanii Vanessa Mdee pamoja na Malaika.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com